Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kutekeleza kwa mafanikio makubwa sera ya Taifa ya kupeleka umeme vijijini kwa asilimia 100, hususan katika Wilaya ya Pangani. Haya yameelezwa leo, Septemba 9, 2024, na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Gift Isaya Msuya, wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha Jaira.
Mhe. Gift alieleza, *"Sote tunafahamu kuwa vijiji vyote 33 vya Wilaya ya Pangani tayari vina umeme. Hii inaonyesha dhahiri kuwa Rais wetu anaendelea kuhakikisha umeme unaunganishwa kila kijiji na kila kitongoji."*
Kwa mujibu wa maelezo yake, awamu ya pili ya mradi wa usambazaji umeme itahusisha kila kitongoji. Wananchi wamehimizwa kujiandikisha mapema na kulipia gharama za awali pindi mkandarasi atakapofika katika maeneo yao, ili kila mmoja aweze kufaidika na mradi huu muhimu wa maendeleo.
Aidha, Mhe. Gift alitoa rai kwa wananchi kujiepusha na kuchoma moto maeneo yenye nguzo za umeme, kwani jambo hilo linaweza kuathiri miundombinu na kurudisha nyuma juhudi za serikali za kuleta huduma za umeme vijijini.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa