DKT SAMIA KULETA NEEMA KWA WAVUVI WILAYA YA PANGANI .
Pangani _ Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kuboresha miundombinu mbalimbali nchini.
Katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, imepanga kutekekeza Mradi wa ujenzi wa soko la Kimataifa la samaki kijiji cha Kipumbwi.
Mradi huo utakuwa na thamani ya TZS bilioni 1.5 ambapo kwa sasa Wizara ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha michoro ya soko hilo kisha itatangaza tenda ya ujenzi.
Mradi huo utachangia kuongeza kipato kwa jamii na ajira kwa wazawa wa Pangani, kwani soko hilo linatarajiwa kuwa na miundombinu muhimu, kama vile, mitambo ya kuzalisha barafu, vyumba vya ubaridi (cold rooms) ili kuhifadhia samaki, eneo la kuhifadhia dagaa (stoo/ghala) eneo la Mama lishe, Parking ya Magari n.k
Sambamba na hilo, Chama cha ushirika cha wavuvi na wafanya biashara wa mazao ya uvuvi Kipumbwi kimejengewa chanja kumi (10), za kuanikia dagaa katika mradi wa majaribio kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Chuo Cha Mipango na wafadhili kutoka Japan (JAICA).
Hayo yamesemwa leo Julai 10, 2024 na mkuu wa Wilaya ya Pangani mhe Mussa Kilakala wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa kata ya Kipumbwi Wilayani Pangani
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa