Kamati ya afya ya msingi (Primary Health Care) imeketi na kujadili kuhusu kampeni ya mtu ni afya pamoja na kutoa elimu ya ugonjwa wa Mpox.
Hayo yamefanyika leo Septemba 2, 2024, katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya Ugonjwa wa Mpox, afisa afya kutoka Hospitali ya Wilaya bi Mwanahamisi Ramadhan amesema, Ugonjwa wa Mpox husababishwa na virusi vya monkeypox, na unaambukizwa kwa njia ya maji maji ya mwili, mfumo wa njia ya hewa na ngozi ya mgonjwa kupitia kugusana na kujamiana
Ameongeza kuwa dalili kuu ya Mpox ni upele wa melengelenge au vidonda vinavyoweza kuathiri uso, viganja vya mikono nyayo za miguu na sehemu za siri
Aidha amefafanua kuwa ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa kulazwa, kupatiwa tiba ya dalili, dawa ya kutibu kirusi pamoja na kupunguza ukali wa vipele.
Sambamba na hilo amesema kuwa hatua za kujikinga na ugonjwa huu ni kuepuka kugusana na mgonjwa wa Mpox ikiwemo kujamiiana, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kuwahi katika vituo vya huduma za afya, kuepuka kugusa nyama na damu za wanyama pori wanaougua na kupika vizuri mazao ya nyama kabla ya kula.
Kikao kimewakutanisha , Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri, Kamati ya Usalama (W), Viongozi wa dini, pamoja na wasimamizi wa Shughuri za Afya.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa