Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, chini ya uongozi wa Mwenyekiti Mhe. Akida Bahorera, leo tarehe 20 Januari 2025, imekagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Katika ziara hiyo, kamati ilitembelea mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mwembeni, ambao hadi sasa unaendelea vizuri.
Kamati ilipongeza usimamizi mzuri wa mradi na kumtaka mkandarasi kuongeza juhudi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyopangwa.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa