Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo Januari 8, 2025 imeketi na kujadili Maandalizi ya awali ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na vipaumbele vya lishe kwa sekta mtambuka.
Kikao hicho kimeketi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri (Mkoma),na kimehudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa sekta mtambuka ya Lishe, ikiwemo idara ya Elimu Awali na Msingi, Elimu Sekondari, Maendeleo ya Jamii, idara ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na afisa Lishe mkoa wa Tanga bi Sakina Mustafa.
Akiwasilisha maandalizi ya mpango wa bajeti ya lishe kwa mwaka 2025/2026 afisa lishe Wilaya ya Pangani ndg Daudi Mwakabanje amefafanua kuwa mpango wa bajeti wa utekelezaji wa afua za lishe umezingatia vipaumbele vyote vilivyowekwa kwenye Mpango mtambuka wa Lishe kitaifa wa mwaka 2021-2026(NMNAPII).
Kwa upande wake bi Sakina ambaye ni Afisa Lishe Mkoa wa Tanga ,amebainisha kuwa lishe ni msingi wa uchumi, maendeleo na afya ya binadamu.
"Tumefanikiwa kupunguza tatizo la udumavu kwa mwaka 2018 hadi 2022 toka asilimia 34 hadi 24.1 katika mkoa wetu" . Alibainisha.
Aidha amefafanua mfano wa afua za kutekeleza kwa mwaka 2025/2026 ikiwemo kutoa elimu ya lishe kwa jamii, kuzingatia mlo kamili, ukaguzi wa vyakula, pamoja na ufuatiliaji wa moja kwa moja katika jamii juu ya masuala ya lishe.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa