KAMATI YA LISHE YAKETI KUJADILI UTEKELEZAJI WA AFUA ZA LISHE, KIPINDI CHA ROBO YA TATU 2024/2025.
Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo Aprili 16, 2025 imefanya Kikao cha kawaida cha Kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha Robo ya Tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2025.
Akifungua kikao hicho kaimu Mkurugenzi Mtendaji, ndug Juma Mbwela amesema kuwa kikao hichi ni muhimu sana kwani Halmashauri yetu inaendelea kutekeleza maagizo ya upatikanaji wa lishe kwa vitendo, Serikali ya awamu ya sita imeendelea kulipa umuhimu wa kipekee suala la lishe bora katika jamii.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndugu Daudi Mwakabanje amesema kuwa Divisheni ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii imeendelea kutekeleza afua za Lishe na kufanikiwa kutoa elimu kwa Wananchi kupitia vikao mbalimbali kuhusu masuala ya lishe bora.
" Katika kipindi cha robo ya tatu, tumefanikiwa kutekeleza afua za lishe kwa kutumia kadi alama, ambapo tumepima viashiria mbalimbali ikiwemo kiashiria cha upimaji wa utapiamlo, kiashiria cha utoaji wa chakula Shuleni angalau mlo mmoja, kiashiria cha usimamizi shirikishi". Alisema.
Sambamba na hilo Idara mbalimbali ziliwasiliisha taarifa za utekelezaji wa Afua za lishe kwa kipindi cha robo ya tatu ikiwemo idara ya Elimu ya Awali na Msingi, Idara ya Elimu Sekondari, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Idara ya Mipango na Uratibu.
Aidha, katika kikao hicho wajumbe walitoa ushauri juu ya masuala ya Lishe bora na kuzingatia usafi pamoja na kukubaliana kuendelea kutoa hamasa na elimu kwa wananchi juu ya masuala ya lishe ili kuendelea kuboresha hali ya lishe katika Wilaya ya Pangani wa ujumla.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa