Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Pangani (DCC) leo Machi 4, 2025 imefanya kikao kujadili na kupitisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2025/2026.
Akifungua kikao hicho kilichoketi katika ukumbi wa Halmashauri ya zamani, Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Gift Isaya Msuya ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao hicho aliwataka wajumbe kujadili rasimu ya mapendekezo ya mpango na bajeti kwa makini kwa maslahi mapana ya Halmashauri.
Akiwasilisha taarifa ya rasimu ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri Afisa Mipango Wilaya ya Pangani ndg Simeon Vedastus amesema kuwa kwa asilimia kubwa Serikali imetekeleza wajibu wake wa uletaji fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
" Tumepata fedha kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Zahanati zetu, fedha za ujenzi wa nyumba ya mwalimu Shule ya Sekondari ya Jumaa Aweso, Ukarabati wa Vyumba vya Madarasa, ujenzi wa Bweni shule ya Sekondari Funguni, kumalizia ujenzi wa sekondari ya Bweni pamoja na Mwera, ujenzi wa nyumba ya afisa kilimo". Alifafanua
Aidha aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Wilaya ya Pangani inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha Tshs Billioni 23.9 ikijumuisha Mishahara, Matumizi Mengineyo, Mapato ya Ndani pamoja na miradi ya maendeleo.
Kamati hiyo pia imepata fursa ya kufanya mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 na mwaka wa fedha 2024/2025 kwa kipindi cha kuishia Desemba 2024.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa