KARAKANA YA KISASA YATOA MATUMAINI KWA VIJANA PANGANI.
Pangani, Tanga
Shule ya Msingi Pangani imepata karakana mpya ya kisasa ya mafunzo ya ufundi kupitia Mradi wa IPOSA unaofadhiliwa na KOICA kutoka Korea Kusini.

Aidha Karakana hiyo ina ukumbi wa mafunzo kwa vitendo, stoo, ofisi, pamoja na matundu mawili ya vyoo.
Vilevile karakana hiyo ina mashine ya kisasa ya kurandia mbao, mashine za chelehani 15 na vifaa vingine vya useremala na ushonaji vitakavyo saidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Lengo kuu la mradi huu ni kuwapa vijana ujuzi wa mikono na kuwafungulia njia ya kujitegemea kimaisha kwa kuwawezesha vijana kujifunza ushonaji na useremala.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa