Na Martin Kamote, Pangani_ Tanga.
Katibu Mkuu wizara ya Kilimo, bw. Gerald G Mweli leo tarehe 17 Aprili, 2025, amezindua rasmi nyumba ya Afisa Ugani Kilimo iliyopo Kata ya Masaika, Kijiji cha Masaika Wilayani Pangani.
Katibu Mkuu Mweli amesema kuwa ni wakati sahihi kwa maafisa ugani kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuhakikisha wanatoa ushauri bora katika kuhakikisha wanapata matokeo chanya.
Bw. Gerald Mweli amesema kuwa " hakika yanayofanyika Pangani ni mambo ya kupongeza sana, tumekuwa na changamoto ya nyumba za maafisa ugani kwa muda mrefu sana, lakini tunashukuru mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo , hivyo nawapongeza sana kwa matokeo mazuri ya mradi huu" . Alisema.
Aliongeza kuwa maafisa ugani wanapaswa kufanya kazi bora kwa kuhakikisha utoaji wa huduma za kilimo zinafanyika kwa wananchi.
Aidha amempongeza mbunge wa jimbo la Pangani ambae pia ni waziri wa Maji mhe Jumaa Aweso kwa kufuatilia kwa karibu nyumba hii, hadi kukamilika, hivyo mbunge wa jimbo hili amefanya kazi kubwa sana.
Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekusudia kujenga nyumba kwa maafisa ugani nchi nzima pamoja na ununuzi wa matrekta ili kurahisisha huduma kwa wananchi wote.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa