KIKAO CHA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE.
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo tarehe 20 Novemba 2023 imefanya kikao cha tathmini ya Lishe kilichofanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri.
Akisoma taarifa ya Lishe Afisa lishe Wilaya ndugu Daud Mwakabanje, amesema kuwa taarifa ya hali ya lishe katika Wilaya inaonesha kuwa jumla ya watoto 5258 wapo katika hali nzuri ya lishe, ambapo watoto jinsia ya kiume 2594 wapo kwenye hali ya Kijani, na 2659 jinsia ya kike wapo kwenye hali ya kijani na watoto 5 pekee ambao wapo kwenye hali ya njano, na tayari wamepatiwa njia bora ya kuzingatia Lishe.
Kwa upande wake Afisa Tarafa wa kata ya Madanga bw Ismail Mwandege ambae amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya amewataka watendaji wa kata katika Halmashauri kuweka jitihada za kutoa elimu ili kuondoa matatizo na magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora haswa kwa watoto walio chini ya miaka mitano.
"Lishe bora kwa mtoto huimarisha Afya na kumpa nguvu mtoto ili aweze kutimiza shughuli zake za kila siku, mtoto mwenye Afya nzuri mara zote anakuwa na furaha hata kwa kumuangalia tu anaonekana anapendeza"Alisema.
Hata hivyo kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii Bw. Kirigiti Matera amesema kuwa ni muhimu Afisa Lishe kutembelea vituo vyote vya Mahitaji maalumu kwaajili ya kutoa elimu ya lishe na Shule zote za Chekechea(Day care) ndani ya wilaya ya Pangani, kupatiwa elimu ya Lishe bora.
Kikao cha Tathmini ya Lishe kwa watendaji ni vikao endelevu vinavyofanyika kila robo katika mwaka, ili kujua mwenendo mzima wa lishe kwa watoto katika Halmashauri ikiwa na lengo la kuhakikisha watoto wote wanakuwa na Afya njema.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa