Pangani_Tanga
"Lishe bora kwa Vijana Balehe, Chachu ya Mafanikio yao".
Hii ni kauli mbiu iliyobeba dhana nzima ya maadhimisho ya siku ya Lishe Kitaifa, iliyofanyika Leo Oktoba 27, 2023 ,Kiwilaya katika ofisi ya Kata iliyopo Pangani Magharibi, na kuhudhuliwa na watalaamu mbalimbali wa Afya.
Maadhimisho haya yamehusisha upimaji wa uwiano wa Urefu na uzito(BMI) kwa vijana balehe ambapo zoezi hilo limeongozwa na wataalamu wa Afya kutoka Hospitali ya Wilaya ya Pangani kwa kushirikiana na Afisa Lishe wa Wilaya ndg Daud Mwakabanje.
Hata hivyo kwa upande wake Afisa Lishe( W) Bwana,Daudi Mwakabanje, ameendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kuwapa watoto vyakula vinavyozingatia mlo kamili ikiwa ni pamoja na kuwanyonyesha watoto maziwa ya mama kwa pekee ndani ya miezi sita ya mwanzo.
Kwa upande wake ndg Roita Mponji ambae alisimama kwa niaba ya Mgeni rasmi ameendelea kusisita juu ya umuhimu wa kuzingatia Lishe bora
" Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kuimarisha afya za watanzania kwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa afua za lishe kwa kupunguza madhara ya kiafya yatokanayo na lishe duni kwa jamii; Madhara hayo ni udumavu, uzito pungufu, ukondefu uzito uliopitiliza, upungufu wa damu na kutokomeza utapiamlo mkali hususani kwa Watoto chini ya miaka mitano".
Halmashauri ya Pangani imendelea kupiga hatua katika utekelezaji wa afua za lishe na hivyo kupungua kwa kiasi kikubwa kwa matatizo ya kiafya yatokanayo na lishe duni, mathalani udumavu 1%,Upungufu wa damu kwa akina mama wajawazito 4.7%,Ukondefu 0.8% na uzito uliopita kiasi 0.2%; hali ambayo ni himilivu ukilinganisha na asilimia za kitaifa.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa