Maafisa watendaji wa kata 6 za Halmashauri ya wilaya ya Pangani wamekabidhiwa pikipiki 6 kati ya pikipiki 916 zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa ajili ya watendaji kata nchini lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Katika mgao wa awamu ya kwanza Pikipiki hizo zimetolewa kwa kata 6 kati ya kata 14 za Wilaya ya Pangani. Mgao huo umefanyika Kwa kuzingatia Kata zilizopo pembezoni na yenye vijiji vingi, Kata hizo ni Kata ya Mkalamo, Mkwaja, Masaika, Mikunguni, Kipumbwi na Bushiri.
Zoezi la Kukabidhi pikipiki kwa Maafisa watendaji wa kata limefanyika Wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani la kupitisha Bajeti ya Halmashauri 2023/2024. Hivyo kufanya zoezi hilo kuudhuriwa na Wah. Madiwani wa kata zote 14 za Halmashauri ya wilaya ya Pangani, Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri, Mwenyekiti(W) na Katibu(W) wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mhe. Kaimu Mkuu wa wilaya, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi. Pamoja na Wananchi waliohudhuria Baraza hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mhe. Akida Omari Bahorera na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Ndg. Isaya M. Mbenje wameogoza zoezi hilo la Kukabidhi pikipiki kwa maafisa watendaji kata.
Viongozi hao wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kugawa pikipiki hizo kwa Maafisa watendaji wa kata ili kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Pia Viongozi hao wamewaelekeza Maafisa hao Kutumia Pikipiki hizo kwa ajili ya kazi iliyokusudiwa na serikali ya kuwahudumia wananchi huku wakiwasisitiza kuzitunza na kuzithamini kwa kutambua kuwa ni mali ya Umma.
Aidha Maafisa watendaji kata hao wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mgao huo wa pikipiki na kuhaidi kutumia pikipiki hizo kwa matumizi mazuri ya kiofisi ili kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuleta maendeleo.
Pangani DC
Kazi Iendelee✍✍
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa