Pangani -Tanga.
Leo Januari 8, 2025 shughuli za matibabu ya macho na upasuaji zimeendelea kutolewa katika hospitali ya Wilaya ya Pangani ambapo zoezi hilo litadumu kwa siku Saba na kuhitimishwa Januari 10, 2025.
Huduma hiyo inatolewa na Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya care association kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa hospitali ya Wilaya ya Pangani kutoa matibabu hayo bure kwa wananchi wote.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo linalo endelea Mganga mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Pangani,Dkt Hassan Msafiri amebainisha kuwa
"Kipekee nachukua fursa hii kuishukuru taasisi hii kwani imekuwa ni fursa kwetu ya kujifunza na kuongeza ujuzi kwa wataalamu wetu wa hospitali ya Wilaya ya Pangani ikiwa mpaka sasa tumeweza kufanya upasuaji wa wagonjwa wa goita na upasuaji wa mtoto mdogo chini ya miezi sita na umefanikiwa kwa asilimia mia". Alibainisha.
Sambamba na hilo Dkt Msafiri ametoa shukrani zake kwa mbunge pamoja na mkuu wa Wilaya ya Pangani Kwa kutoa ushirikiano lakini shukrani za dhati Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.MH DKT Samia Suluhu Hasani kwa kuipa kipaumbele sekta ya Afya kwa ujumla.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa