Hayo yamefanyika leo Septemba 26, 2024, wakati Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Pangani ndg Charles Edward Fussi, alipotoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika ifikapo Novemba 27, 2024.
Ndugu Charles Edward Fussi, ametoa maelezo hayo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ambapo ametoa wito kwa Wananchi wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
" Kwa mujibu wa Tangazo la Uchaguzi lililotolewa kwa kuzingatia kanuni ya 4 ya kanuni za uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa( Tangazo la Serikali na 571) Uchaguzi Utafanyika tarehe 27 Novemba 2024". Alisema
Pia ameongeza kwa kutoa wito kwa wananchi kutumia Demokrasia yao kushiriki kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura ili waweze kuchagua viongozi wao wanaowapenda, pasipo vurugu ya aina yoyote.
Aidha katika zoezi hilo makundi mbalimbali yamepata nafasi ya kushiriki zoezi hilo muhimu la kupokea maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na kupata nafasi ya kutoa maoni mbalimbali yenye lengo la kuboresha mchakato mzima wa uchaguzi huo.
Makundi hayo yamejumuisha viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, waandishi wa habari, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi, Wananchi mbalimbali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama, ambapo kwa pamoja ,wameahidi kushiriki kwa haki na kuzingatia sheria katika zoezi hilo kuanzia ngazi ya uandikishaji hadi upigaji kura.
Kauli mbiu " Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa