Mwenge wa Uhuru umekagua na kuridhishwa na mradi wa ujenzi wa Vyumba (4) vya Madarasa pamoja na Matundu 7 ya Vyoo kwaajili ya Kidato cha 5 & 6.
Hayo yamefanyika Aprili 16,2024 katika Shule ya Sekondari Funguni iliyopo kata ya Pangani Magharibi, ambapo jumla ya Shilingi milioni 116 fedha kutoka Serikali kuu zimetumika kukamilish a mradi huo.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo mkuu wa Shule hiyo ndugu Gamba amesema kuwa " Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ujenzi wa mradi huu, kwaajili ya mapokezi ya kidato cha 5."
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu Godfrey Mnzava amesema kuwa_:
" Mwenge wa Uhuru umerizika na kuzindua mradi huu kwani kazi nzuri imefanyika".
#Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa