Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imeendelea na mkakati wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Hayo yamefanyika leo tarehe 27/02/2024 katika kikao cha kimkakati cha umezeshaji dawa kinga za Minyoo Tumbo Mashuleni kilichoongozwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya Afisa Tarafa ndg Helswida Majula kwenye ukumbi wa zamani wa Halmashauri.
Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTD) Wilaya ya Pangani, Dkt. Jumanne Akilimali, alibainisha aina za magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele hususan Minyoo Tumbo.
Dkt.Akilimali ameongeza kuwa, ili kukabiliana na tatizo hilo Wilaya ya Pangani kwa kushirikiana na wizara ya Afya itaendesha zoezi la utoaji wa Dawa kingatiba kwa watoto wa umri kuanzia miaka 5 hadi miaka 14 wa shule zote ambapo zoezi hilo litaanza siku ya kesho tarehe 28/02/2024.
Aidha,aliongeza kuwa zoezi hilo litasimamiwa na walimu wakishirikiana na watumishi wa Afya na lengo ni kuwafikia wanafunzi 16,000.Hii itasaidia kuondokana na changamoto za udumavu, utapiamlo na upungufu wa damu unaokabili kundi hilo la wanafunzi ambao wengi ni wahanga wa Minyoo Tumbo.
Wizara ya Afya imeendelea na mpango mkakati wa kusambaza kingatiba kwa wananchi wote ili kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo matende, mabusha, vikope, kichocho, minyoo na Usubi
#"meza kingatiba za minyoo kila inapotolewa Shuleni na kwenye jamii"#.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa