Halmashari ya Wilaya ya Pangani leo Juni 10, 2024, imefanya bonanza la lishe katika kijiji cha ubangaa.
Aidha katika bonanza hilo shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo maazimisho ya Siku ya Afya na Lishe, kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia pamoja na kufanya michezo.
Sambamba na hilo Afisa Lishe( W) ndg Daudi Mwakabanje ametoa rai kwa wananchi na kuwataka kuendelea kushiriki na kutekeleza kwa vitendo afua za Lishe kwa watoto,Vijana wa rika balehe pamoja na Wazee.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii ndg Kirigiti Matera, amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuwalinda na kutetea haki za watoto na kuripoti matukio yoyote yanayohusu ukatili wa kijinsia.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa