Mkuu wa idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ndg Ramadhani Zuberi ( katikati) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ndg Charles Edward Fussi, leo Oktoba 29, 2024 ameongoza kikao cha kamati ya lishe kujadili tathimini ya Mkataba wa Lishe kwa Robo ya Kwanza kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2024/2025 katika Ukumbi wa CTC Hospitali ya Wilaya ya Pangani.
Akiwasilisha taarifa ya Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, kaimu Afisa Lishe Wilaya ndg Ibrahim Mohamed amesema kuwa
" katika robo ya kwanza Divisheni ya lishe imefanikiwa kutekeleza afua mbalimbali kama vile kushiriki katika utoaji wa Huduma za Afya mseto, kufanya tathimini ya hali ya lishe kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutoa elimu na unasihi wa lishe, kufanya matibabu ya utapiamlo mkali kwa watoto wachanga,kufanya Maadhimisho ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama duniani, kufanya ukaguzi wa vyakula , tathmini ya hali ya lishe kwa wananchi kwa kutumia kipimo cha uwiano wa uzito kwa urefu(BMI) pamoja na kufanya Maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe ya Kijiji ( SALiKi), ". Alisema
Taarifa zingine zilizojadiliwa ni kadi alama kwa ngazi ya kata na Halmashauri pamoja na viashiria mbalimbali vya lishe ambavyo vipo kwenye ilani ya chama Tawala ambapo afisa lishe amebainisha kuwa tuko vizuri kwa asilimia zote 100, na kuendelea kutoa elimu katika jamii.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa