Pangani_ Tanga
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Sea Sense imetambulisha mradi wa kuhifadhi viumbe wa baharini walio katika hatari ya kutoweka Duniani, ikiwemo kasa pamoja na nguva.
Hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ambapo mada mbalimbali kuhusu uhifadhi wa viumbe hao ziliwasilishwa na wataalam kutoka East Africa crude oil pipeline ambapo alieleza faida za uhifadhi wa viumbe wa baharini na kutoa elimu kwa jamii katika pwani ya bahari ya Tanga.
Aidha ndg Joshua Afata alifafanua kuwa sababu ya kuleta mradi huu katika mkoa wa Tanga ni pamoja na Tanga ni sehemu ambayo mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki unatekelezwa hivyo ni sehemu ya Utekelezaji wa mpango wa tathmini kuhusu athari za kimazingira na kijamii zinazoweza kujitokeza alifafanua.
"Madhumuni ya mradi huu ni kutambua hali ya kasa wa baharini na nguva na matishio yanayohusiana na maisha yao katika mazingira ya bahari ya Tanga".
Sambamba na hilo amebainisha wadau katika mradi huo ikiwa ni pamoja na PRO RALG(TAMISEMI), Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani,Serikali za Mitaa, kata na vijiji, vikundi vya Mazingira vya jamii (BMUs), pamoja na wawekezaji sekta binafsi ikiwemo hoteli na utalii wa pwani.
#tulindeviumvevyabahari.
#okoakasa,okoanguva.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa