Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imeendelea kunufaika na Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), wenye lengo la kuboresha Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia katika Shule za Sekondari.
Timu ya uthibiti ubora wa Shule ikiongozwa na bwan Frank Maeda imefanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo Novemba 7,2023, katika Shule ya Sekondari Masaika iliyopo kata ya Masaika Wilayani Pangani na kuonyesha kuridhishwa na maendeleo ya jenzi wa Shule hiyo uliotekelezwa kwa jumla ya Shilingi Milioni 584, Fedha kutoka Serikali kuu,kupitia SEQUIP.
Bwana Maeda ameongeza kwa kuipongeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, pamoja na usimamizi mzuri wa Mkuu wa Wilaya mhe Zainab Abdallah na wataalamu wote waliojitoa katika utekelezaji wa mradi huu.
" Madhumuni ya mradi huu ni kuongeza ufikiwaji wa elimu ya sekondari, kuwapatia wasichana mazingira bora ya kujifunza na kuboresha uhitimu bora wa elimu ya sekondari kwa wasichana na wavulana".
Ikumbukwe kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ilitoa miongozo ya ujenzi wa shule hizi katika Halmashauri zote nchini na kuziagiza kukamilisha ujenzi wa shule hizi mapema ili ziweze kutoa huduma kwa wanafunzi na kuboresha Elimu.
Shule hii inatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza ifikapo januari 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Panagani inaendelea kumshukuru Rais .Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya Elimu katika Wilaya ya Pangani.
#panganimpya
#elimubora
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa