Shirika la IPOSA (Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Shule) limefadhili mradi mkubwa wa maendeleo katika Shule ya Msingi Pangani.
Aidha mradi huu unahusisha ujenzi wa kalakana mpya pamoja na ujenzi wa choo matundu 2
Lengo kuu ni kuwapa vijana ujuzi wa mikono na kuwafungulia njia ya kujitegemea kimaisha kwa kuwawezesha vijana kujifunza ushonaji na useremala.
Vilevile mradi huu unawalenga vijana walioacha shule, wale waliomaliza darasa la saba bila kuendelea, na hata ambao hawajawahi kabisa kupata nafasi ya kwenda shule kuanzia umri wa miaka 14 na kuendelea.
Hadi sasa mradi huu umetumia shilingi milioni 54 ambapo kwa sasa hatua za upakaji rangi zinaendelea.
Tunashukuru Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo IPOSA kwa uwekezaji huu wa maana unaogusa maisha ya vijana wetu.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa