Tuongeze Kasi ya Utoaji Elimu na Upimaji wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu.
Hayo yamesemwa leo tarehe 17 Januari 2025, na timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya Wilaya ya Pangani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na Ukoma kwa haraka.
Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Soko kuu la Pangani ambapo mtaalamu kutoka Hospitali ya Wilaya ambaye ni mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma, Dkt. Abdallah Usi, amebainisha kuwa Kifua Kikuu husababishwa na bakteria au viini, na kwa kawaida hushambulia mapafu.
Dkt. Usi ameongeza kuwa viini vya TB vinaweza kushambulia sehemu yoyote ya mwili, kama vile figo, mgongo, au ubongo. Lengo la kampeni hii ni kutoa huduma ya upimaji na matibabu bure kwa wananchi ili kupunguza maambukizi na kuokoa maisha kwani kifua kikuu kinatibika.
Sambamba na hilo dkt Usi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Hospitali ya Wilaya kupata kipimo bora cha kupimia na kuhakikisha wananchi wote wanaobainika kuwa na ugonjwa wa kifua kukuu (TB) wanapimwa na kupewa matibabu bila malipo yeyote.
Aidha, katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya uchunguzi wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma, ulitoa fursa kwa wananchi kupima na kutambua hali zao za afya bure, na kuanzishwa matibabu bila malipo yeyote na kutoa rai kwa jamii kutowaficha wale wote wenye dalili ya ugonjwa huo
Kampeni hii yenye lengo la kuendelea kuboresha huduma za afya na kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu hatari itahitimishwa tarehe 24 Jan
uari 2025.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa