Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa Kushirikiana na Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa nafasi kwa wananchi kuwachagua au kuwapigia kura Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii waliomba kujitolea kwenye Vitongoji vyao vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Wahudumu hao watatambuliwa kupitia Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii.
Zoezi la upatikanaji wa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii limefanyika leo Septemba 10,2024 katika kitongoji cha Kisondo, kijiji cha Mwera Wilayani Pangani, ambapo zoezi la upatikanaji wa Wahudumu hao limefanyika
Aidha wananchi wa kitongoji hicho walipata fursa ya kuwapigia kura Wahudumu hao.
Kwa upande wake afisa mradi kutoka shirika la Amref ameshiriki zoezi la wazi la uchaguzi huo na amefafanua kuwa _:
" Amref kupitia ufadhiri kutoka ubalozi wa Iland inatekeleza mradi huu Wilayani Pangani wenye lengo la kutoa Elimu ya Afya, mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya Lishe kwa jamii ". Alisema.
Sambamba na hilo ndg Bahati Mwailafu kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa kwa kushirikiana na Mdau wa Maendeleo Shirika la AMREF amesema kuwa Wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapo muda mrefu na Serikali imeendelea kuboresha kwa kutekeleza Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, ambapo kila Mtaa na Kitongoji kutakuwa na Wahudumu wawili (Me na Ke)
" Wahudumu tuliowachagua watapewa mafunzo ndani ya miezi sita na watakuja kutoa huduma katika maeneo yetu" .
Hata hivyo kwa upande wake ndg Hamza Mohamedi ambae amepata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mhudumu wa afya ngazi ya jamii ameishukuru Serikali kupitia mradi huu na kuahidi kujituma ili kuleta mafanikio katika jamii.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa