Halmashauri ya wilaya ya Pangani mkoani Tanga Leo imegawa vishikwambi (tablets) zipatazo 221, kwa makundi ya walimu wa shule za msingi na sekondari , waratibu elimu kata pamoja na maafisa elimu ngazi ya halmashauri.
Ugawaji wa vishikwambi hivyo uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani ulizinduliwa na Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Mh Hassani Bakari Nyange. Ambaye ni Katibu tawala wilaya ya Pangani.
Akizungumzia zoezi hilo, afisa elimu msingi wilaya ya Pangani Bwana Juma Hassan Mbwela ameishukuru serikali kwa kutoa vishikwambi kwakuwa vitasaidia kuboresha elimu wilayani Pangani.
Mwl. Mbwela amewataka walimu waliopata vishikwambi hivyo kuvitumia kulingana na matumizi yanayolengwa katika ufundishaji akiwasisitiza kutovitumia kwa matumizi yasiyolengwa.
Kwa upande wao baadhi ya walimu wameishukuru serikali kwa kuwapatia vishikwambi hivyo wakiahidi kuvitumia katika njia bunifu za ufundishaji zitakazosaidia wanafunzi kujifunza kuelewa kwa urahisi.
Kwa ujumla Idadi kamili ya vishikwambi inayohitaji kutolewa ni 372 hivyo kutolewa vishikwambi 221 ni pungufu ya vishikwambi vipatavyo 151 ambavyo vinatarajiwa kuongezwa kutoka Mkoa wa Dar Es Salam kwa ajili ya kuwapatia walimu waliokosa kwa awamu ya kwanza.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa