Leo Septemba 30,2024 wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, ngazi ya kata na Vijiji, wamepatiwa mafunzo ya Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, kutoka kwa waratibu wa uchaguzi ngazi ya Wilaya.
Hayo yamefanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, ambapo Mratibu wa uchaguzi ngazi ya Wilaya Wakili Msomi ndg Agape Fue, amebainisha kanuni zitakazoongoza uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
" Uchaguzi huu utaongozwa na Kanuni zifuatazo, Kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji, katika Mamalaka za Wilaya ( Tangazo la Serikali na. 571 la Mwaka 2024)". Alifafanua.
Aidha Wakili Fue amewataka wakazi wenye umri wa miaka ishirini na moja au zaidi wanaotaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa Kijiji, Ujumbe wa Halmashauri ya Kijiji, au Uenyekiti wa Kitongoji kuchukua fomu za kugombea zinazopatikana kwenye ofisi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
Sambamba na hilo amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili wawe na uelewa wa kutosha katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Mada nyingine zilizo wasilishwa na waratibu wa uchaguzi ngazi ya Wilaya ni pamoja na matumizi ya fomu mbalimbali za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, maadili ya Utumishi wa umma kwa watumishi wanaohusika katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, upokeaji na utunzaji wa vifaa vya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, tehama,uhamasishaji wa Wananchi kushiriki shughuli zote za uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, kuhabarisha unma juu ya masuala ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uandaaji wa Taarifa za uchaguzi.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa