Wizara ya Afya imekabidhi Mashine ya kuchanganyia madini joto kwenye chumvi yenye thamani ya shillingi milioni 18 kwa wanakikundi wanaojihusisha na uzalishaji wa chumvi Kijiji Cha Sange Wilayani Pangani.
Akikabidhi mashine hiyo, Afisa Lishe Muandamizi kutoka ofisi ya Rais Tamisemi Bi,Hamida leo Februari 1, 2025, amewataka wanakijiji kuzingatia utunzaji na usimamizi mzuri wa Mashine hiyo.
" Tutunze Mashine hii ili iweze kudumu Kwa muda mrefu na kuleta manufaa kwa mwanakikundi kwa ujumla,hasa katika kuboresha Afya na Lishe ". Alifafanua
Kwa upande wake Afisa lishe Mkoa wa Tanga Bi ,Sakina Mustafa amesema kuwa Mashine hiyo Ina thamani kubwa sana na malengo yake ni kuona Kijiji Cha sange wanazalisha chumvi yenye madini joto kwa kiwango chenye ubora.
Lakini pia ametoa elimu juu ya uchanganyaji sahihi wa madini joto kwenye chumvi na kuwataka kuacha kutumia njia asili ambazo si rafiki kwa Afya ya mwanadamu.
Akipokea mashine hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bi, Jenifa amesema
"Tunashukuru kwa mashine hii ambayo itaenda kuzalisha chumvi yenye ubora Mnahaja ili kuweza kupandisha thamani ya bidhaa hiyo.
Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Pangani ni moja kati ya Wilaya 33 Tanzania zenye uwezo wa kuzalisha chumvi kwa kiasi kikubwa .
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa