Zaidi ya Wanafunzi 398 wamejengewa uwezo wa kupambana na ukatili wa kijinsia Wilayani Pangani.
Wanafunzi hao wameahidi kuwa mabalozi wazuri katika kuendelea kupambana na vitendo viovu katika jamii.
Hayo yamebainishwa leo Julai 31,2024 katika Shule ya Sekondari Funguni na mkuu wa Kitengo cha Ustawi wa jamii ndg Thadei Kamisa alipotembelea shuleni hapo na kusema kuwa :_
" Kutokana na ongezeko la matukio na vitendo viovu katika jamii, sisi kama sehemu ya jamii tumeona ni vema tuendelee kutoa elimu mashuleni juu ya ukatili wa kijinsia na namna ya kukabiliana na matukio hayo". Alisema.
Aidha kwa upande wake afisa toka Dawati la jinsia ndg Majid Ally amesema kuwa_:
"tunaelekeza nguvu zaidi kwa wanafunzi ili wajitambue wenyewe na kujua viashiria vya ukatili wa kijinsia na namna ya kukabiliana navyo ikiwa ni pamoja na kushirikiana zaidi na jamii katika kukemea vikali vitendo hivyo".
Nae ndg Enock Kirigiti afisa ustawi wa jamii amesisitiza kuwa zoezi la kuwatembelea wanafunzi mashuleni niendelevu na litaendelea kwa shule zote Wilayani Pangani.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa