Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ikiongozwa na Mweyekiti wa Halmashauri Mhe. Akida Bahorera wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya Halmashauri.
Ziara hiyo imefanyika leo Julai 17,2024, lengo ni kuona utekelezaji wa miradi hiyo na hatua zilizofikia kwa wakati uliokusudiwa kukamilika kwa miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni Pamoja na ukamilishaji wa madarasa 8 yenye Ofisi 3 na Vyoo matundu 30 katika Shule ya Sekondari Pangani Halisi ambapo jumla ya Shilingi milioni 116, fedha kutoka Serikali kuu zimetumika na mradi upo katika hatua za ukamilishaji.
Aidha kwa upande wake Diwani wa kata ya Kimang'a mhe Mwandaro Salim Hassan amebainisha kuwa Shule hii imekuwa msaada mkubwa sana kwani imepunguza umbali ambao mwanzoni wanafunzi walikuwa wakitembea kwaajili ya kupata elimu.
" tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za miradi hii ya maendeleo na tunamshukuru pia mbunge wetu ambae pia ni Waziri wa maji kwa kuendelea kuisemea Pangani". Alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo mhe Akida Boramimi ameelekeza kuwa maagizo yote yaliyotolewa yatekelezwe.
Sambamba na hilo kamati imesisitiza kuhakikisha kuwa mradi huu ukamilike kwa wakati na ubora ili kuendelea kutoa huduma bora.
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa