UTANGULIZI
Mradi wa Ujenzi wa ukuta na upandaji wa miti ya mikoko kando ya Mto Pangani, ulianzishwa kwa lengo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi. Ofisi ya Makamu wa Rais kitengo cha Mazingira ambao ndio wanatekeleza mradi huu kwa ushirikiano na Wilaya ya Pangani. Wilaya yetu ni miongoni mwa Wilaya zilizo athirika na mabadiliko ya tabia nchi. Katika kukabiliana na hali hiyo, juhudi za makusudi zilifanywa na kufanikiwa kupata msaada kupitia ofisi ya Makamu wa Rais chini ya mfuko wa kusaidia nchi zilizochini kimaendeleo (LCDF), Wilaya zingine zinazotekeleza mradi kama huu ni Bagamoyo, Rufiji/Mafia na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Kwa Wilaya ya Pangani mradi huu una sehemu kuu mbili ambazo ni ujenzi wa ukuta wa mto Pangani na upandaji wa miti aina ya mikoko katika kingo za mto
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa