UTALII
Wilaya yetu ina hazina kubwa ya vivutio vya utalii, ambavyo ni fukwe nzuri kandokando ya bahari ya Hindi zenye hoteli za kitalii, hifadhi ya taifa ya Saadani, eneo tengefu la kisiwa cha Maziwe, hifadhi ya kasa wa kijani eneo la Madete , Mkwaja na majengo ya kale ya kihistoria.
MAENEO YA KIHISTORIA
Kivutio kingine ni majengo ya kale yaliyojengwa tangu enzi za utawala wa waarabu katika sehemu za mwambao. Baadhi ya majengo haya hivi sasa yanatumika kama ofisi za serikali. Pia tunajivunia mji wetu wa Pangani kuingizwa katika orodha ya miji mikongwe duniani kwa mwaka 2010 baada ya kutangazwa na shirika la kimataifa ya mambo ya kale (International Council of Museums)
kupata taarifa za maeneoo ya utalii bonyeza hapa UTALII.pdf
Pangani District Council
Sanduku la Posta: 89 Pangani -Tanga
Namba ya Mezani: +255 (0) 27 2630058
Namba ya simu: 0658100588/062289307
Barua Pepe : ded@panganidc.go.tz
Hakimiliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya Pangani .Haki Zote Zimehifadhiwa